Isaiah 34:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Someni katika kitabu cha Mwenyezi-Mungu: “Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana, kila kimoja kitakuwako na mwenzake.” Maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hivyo, roho yake itawakusanya hao wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Angalieni katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na msome: Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana, hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake. Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza, na Roho wake Mtakatifu atawakusanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Someni katika kitabu cha Mwenyezi-Mungu: “Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana, kila kimoja kitakuwako na mwenzake.” Maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hivyo, roho yake itawakusanya hao wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Angalieni katika gombo la BWANA na msome: Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana, hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake. Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza, na Roho wake atawakusanya pamoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Angalieni katika gombo la bwana na msome: Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana, hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake. Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza, na Roho wake atawakusanya pamoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Someni katika kitabu cha Mwenyezi-Mungu: “Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana, kila kimoja kitakuwako na mwenzake.” Maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hivyo, roho yake itawakusanya hao wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tafuteni katika kitabu cha Bwana, msome! Hawa nyama hakuna hata mmoja wao asiyepatikana, wote hakuna hata mmoja amkosaye mwenziwe; kwani kinywa chake mwenyewe ndicho kilichowaagiza, nayo Roho yake ndiyo inayowakusanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musome katika kitabu cha Yawe: Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana, kila kimoja kitakuwa na mwenzake. Maana kinywa cha Yawe kimeamuru hivyo. Roho yake itawakusanya hao wote.