Isaiah 34:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ameyakasirikia mataifa yote, ameghadhabika dhidi ya majeshi yao yote. Ameyapangia mwisho wao, ameyatoa yaangamizwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu ameyakasirikia mataifa yote; ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote. Atawaangamiza kabisa, atawatia mikononi mwa wachinjaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ameyakasirikia mataifa yote, ameghadhabika dhidi ya majeshi yao yote. Ameyapangia mwisho wao, ameyatoa yaangamizwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA ameyakasirikia mataifa yote; ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote. Atawaangamiza kabisa, atawatia mikononi mwa wachinjaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana ameyakasirikia mataifa yote; ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote. Atawaangamiza kabisa, atawatia mikononi mwa wachinjaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ameyakasirikia mataifa yote, ameghadhabika dhidi ya majeshi yao yote. Ameyapangia mwisho wao, ameyatoa yaangamizwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana amewachafukia wamizimu wote, makali yake yawatokee vikosi vyao vyote; akawatia mwiko, wasiwepo tena, akawatoa, wachinjwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe amekasirikia mataifa yote, amekasirikia majeshi yao yote. Ameyapangia mwisho wao, ameyatoa yaangamizwe.