Isaiah 34:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Upanga utalowa damu na kutapakaa mafuta, kama kwa damu ya kondoo na mbuzi, na mafuta ya figo za kondoo dume. Maana Mwenyezi-Mungu atatoa kafara huko Bosra, kutakuwa na mauaji makubwa nchini Edomu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Upanga wa Mwenyezi Mungu umeoga katika damu, umefunikwa na mafuta ya nyama: damu ya kondoo na mbuzi, mafuta kutoka figo za kondoo dume. Kwa maana Mwenyezi Mungu ana dhabihu huko Bosra, na machinjo makuu huko Edomu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Upanga wa Bwana umeshiba damu, umenona kwa unono, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo waume; maana Bwana ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Upanga utalowa damu na kutapakaa mafuta, kama kwa damu ya kondoo na mbuzi, na mafuta ya figo za kondoo dume. Maana Mwenyezi-Mungu atatoa kafara huko Bosra, kutakuwa na mauaji makubwa nchini Edomu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Upanga wa BWANA umeoga katika damu, umefunikwa na mafuta ya nyama: damu ya kondoo na mbuzi, mafuta kutoka katika figo za kondoo waume. Kwa maana BWANA ana dhabihu huko Bosra na machinjo makuu huko Edomu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Upanga wa bwana umeoga katika damu, umefunikwa na mafuta ya nyama: damu ya kondoo na mbuzi, mafuta kutoka figo za kondoo dume. Kwa maana bwana ana dhabihu huko Bosra, na machinjo makuu huko Edomu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Upanga wa BWANA umeshiba damu, umejazwa mafuta, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo dume; maana BWANA ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Upanga utalowa damu na kutapakaa mafuta, kama kwa damu ya kondoo na mbuzi, na mafuta ya figo za kondoo dume. Maana Mwenyezi-Mungu atatoa kafara huko Bosra, kutakuwa na mauaji makubwa nchini Edomu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana yuko na upanga uliojaa damu, ukapakwa mafuta: ni damu za wana kondoo na za madume, ni mafuta ya mafigo ya madume; kwani iko sikukuu ya tambiko ya Bwana huko Bosira, liko chinjo kubwa katika nchi ya Edomu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Upanga wa BWANA umeshiba damu, umenona kwa unono, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo waume; maana BWANA ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Upanga utajaa damu na mafuta: damu ya kondoo na mbuzi, na mafuta ya figo za kondoo dume. Maana Yawe ana sadaka huko Bosira, kutakuwa mauaji makubwa katika inchi ya Edomu.