Isaiah 34:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyati wataangamia pamoja nao, ndama kadhalika na mafahali. Nchi italoweshwa damu, udongo utarutubika kwa mafuta yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyati wataanguka pamoja nao, ndama dume na mafahali wakubwa. Nchi yao italowana kwa damu, nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nyati watatelemka pamoja nao, na mahasai pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyati wataangamia pamoja nao, ndama kadhalika na mafahali. Nchi italoweshwa damu, udongo utarutubika kwa mafuta yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyati wataanguka pamoja nao, ndama waume na mafahali wakubwa. Nchi yao italowana kwa damu, nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyati wataanguka pamoja nao, ndama waume na mafahali wakubwa. Nchi yao italowana kwa damu, nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nyati watateremka pamoja nao, na ndama pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyati wataangamia pamoja nao, ndama kadhalika na mafahali. Nchi italoweshwa damu, udongo utarutubika kwa mafuta yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Pamoja nao hata nyati wataanguka, nayo madume na manono ya ng'ombe, nchi yao italewa kwa kuzinywa damu zao, nao mchanga utapata nguvu kwa mafuta yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nyati watatelemka pamoja nao, na mahasai pamoja na mafahali, na nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatanoneshwa kwa shahamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbogo wataangamizwa pamoja nao, wana-ngombe pamoja na ngombe dume. Inchi italewa na damu, udongo utashiba kwa mafuta yao.