Isaiah 35:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mchanga wa moto jangwani utakuwa bwawa la maji, ardhi kavu itabubujika vijito vya maji. Makao ya mbwamwitu yatajaa maji; nyasi zitamea na kukua kama mianzi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji, ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi. Maskani ya mbweha walikolala hapo awali patamea nyasi, matete na mafunjo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mchanga ung'aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mchanga wa moto jangwani utakuwa bwawa la maji, ardhi kavu itabubujika vijito vya maji. Makao ya mbwamwitu yatajaa maji; nyasi zitamea na kukua kama mianzi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji, ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi. Maskani ya mbweha walikolala hapo awali patamea majani, matete na mafunjo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji, ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi. Maskani ya mbweha walikolala hapo awali patamea majani, matete na mafunjo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mchanga ung'aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mchanga wa moto jangwani utakuwa bwawa la maji, ardhi kavu itabubujika vijito vya maji. Makao ya mbwamwitu yatajaa maji; nyasi zitamea na kukua kama mianzi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mchanga wenye moto utageuka kuwa ziwa, nayo nchi iliyokufa kwa kiu itatoka visima vya maji. Penye makao na matuo ya mbweha pataota nyasi na matete na magugu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muchanga wa moto katika jangwa utakuwa ziwa la maji, inchi kavu itabubujika vijito. Makao ya imbwa wa pori yatajaa maji; nyasi zitaota na kukomaa kama mianzi.