Isaiah 36:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo mwaka wa kumi na nne wa utawala wa mfalme Hezekia, mfalme Senakeribu wa Ashuru aliishambulia miji yote yenye ngome ya Yuda na kuiteka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda yenye ngome na kuiteka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kumiliki kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo mwaka wa kumi na nne wa utawala wa mfalme Hezekia, mfalme Senakeribu wa Ashuru aliishambulia miji yote yenye ngome ya Yuda na kuiteka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwa Mfalme Hezekia, Mfalme Senakeribu wa Ashuru alishambulia miji yote ya Yuda yenye maboma na kuiteka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda yenye ngome na kuiteka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kutawala kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo mwaka wa kumi na nne wa utawala wa mfalme Hezekia, mfalme Senakeribu wa Ashuru aliishambulia miji yote yenye ngome ya Yuda na kuiteka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa katika mwaka wa 14 wa mfalme Hizikia, ndipo, Saniheribu, mfalme wa Asuri, alipoipandia miji yote ya Wayuda iliyokuwa na maboma, akaiteka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, katika mwaka wa kumi na nne wa kumiliki kwake mfalme Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akapanda ili kupigana na miji yote ya Yuda yenye boma, akaitwaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa kumi na ine wa utawala wa mufalme Hezekia, mufalme Saniharibu wa Asuria aliishambulia miji yote yenye kuta ya inchi ya Yuda na kuinyanganya.