Isaiah 36:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mkuu wa matowashi akawaambia, “Je unadhani bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu wenyewe tu? Maneno yangu ni pia kwa watu wanaokaa ukutani! Muda si muda wao kama vile nyinyi itawabidi kula mavi yao wenyewe na kunywa mikojo yao wenyewe!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yule jemadari wa jeshi akajibu, “Je, bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Je, hakunituma pia kwa watu walioketi ukutani, ambao, kama ninyi, itawabidi kula mavi yao na kunywa mkojo wao wenyewe?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini yule amiri akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma kwa bwana wako, na kwako wewe, niseme maneno haya? Hakunituma kwa watu hawa walio ukutani, ili wale mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mkuu wa matowashi akawaambia, “Je unadhani bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu wenyewe tu? Maneno yangu ni pia kwa watu wanaokaa ukutani! Muda si muda wao kama vile nyinyi itawabidi kula mavi yao wenyewe na kunywa mikojo yao wenyewe!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Amirijeshi akajibu, “Kwani ni kwa bwana wenu na ninyi peke yenu ambao bwana wangu amenituma kusema mambo haya, wala si kwa watu walioketi juu ya ukuta, ambao, kama ninyi, itawapasa kula mavi yao na kunywa mkojo wao wenyewe?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yule jemadari wa jeshi akajibu, “Je, bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Je, hakunituma pia kwa watu walioketi ukutani, ambao, kama ninyi, itawabidi kula mavi yao na kunywa mikojo yao wenyewe?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini yule kamanda akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma niseme, maneno haya kwa bwana wako na kwako wewe? Hakunituma pia kwa watu hawa wanaokaa ukutani, wanaokabiliwa na tisho la kula mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mkuu wa matowashi akawaambia, “Je unadhani bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu wenyewe tu? Maneno yangu ni pia kwa watu wanaokaa ukutani! Muda si muda wao kama vile nyinyi itawabidi kula mavi yao wenyewe na kunywa mikojo yao wenyewe!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkuu wa askari akawajibu: Je? Bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kwako kuyasema haya maneno? Sio kwa watu hawa wanaokaa ukutani watakaokula pamoja nanyi mavi yao na kunywa mikojo yao?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini yule amiri akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma kwa bwana wako, na kwako wewe, niseme maneno haya? Hakunituma kwa watu hawa walio ukutani, ili wale mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule jemadari akawaambia: “Munazani kwamba bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Maneno yangu ni vilevile kwa watu wanaoikaa juu ya ukuta! Bado kidogo wao kama vile ninyi watakula mavi yao wenyewe na kunywa mikojo yao wenyewe!”