Isaiah 36:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Angalieni basi Hezekia asiwahadae akisema kwamba Mwenyezi-Mungu atawaokoeni. Je, kuna yoyote kati ya miungu ya mataifa aliyewahi kuokoa nchi yake mkononi mwa mfalme wa Ashuru?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Msikubali Hezekia awapotoshe asemapo, ‘Mwenyezi Mungu atatuokoa.’ Je, yuko mungu wa taifa lolote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jihadharini, asije Hezekia akawadanganya, akisema, Bwana atatuokoa. Je! Yuko mungu mmoja wa mataifa aliyewaokoa watu wake na mkono wa mfalme wa Ashuru?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Angalieni basi Hezekia asiwahadae akisema kwamba Mwenyezi-Mungu atawaokoeni. Je, kuna yoyote kati ya miungu ya mataifa aliyewahi kuokoa nchi yake mkononi mwa mfalme wa Ashuru?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Msikubali Hezekia awapotoshe wakati asemapo, ‘BWANA atatuokoa.’ Je, mungu wa taifa lo lote ameshawahi kuokoa nchi yake kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Msikubali Hezekia awapotoshe asemapo, ‘ bwana atatuokoa.’ Je, yuko mungu wa taifa lolote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jihadharini, Hezekia asije akawadanganya, akisema, BWANA atatuokoa. Je! Kati ya miungu ya mataifa, kuna yeyote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka katika mkono wa mfalme wa Ashuru?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Angalieni basi Hezekia asiwahadae akisema kwamba Mwenyezi-Mungu atawaokoeni. Je, kuna yoyote kati ya miungu ya mataifa aliyewahi kuokoa nchi yake mkononi mwa mfalme wa Ashuru?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizikia asiwapoteze na kusema: Bwana atatuponya! Je? Miungu ya wamizimu iliweza mmoja tu kuiponya nchi yake, isichukuliwe na mfalme wa Asuri?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jihadharini, asije Hezekia akawadanganya, akisema, BWANA atatuokoa. Je! Yuko mungu mmoja wa mataifa aliyewaokoa watu wake na mkono wa mfalme wa Ashuru?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musimusikilize Hezekia anapowadanganya akisema: ‘Yawe atatuokoa.’ Kuna yoyote kati ya miungu ya mataifa aliyeokoa inchi yake toka katika mikono ya mufalme wa Asuria?