Isaiah 36:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme wa Ashuru alimtuma jemadari mkuu kutoka Lakishi na jeshi kubwa kumwendea mfalme Hezekia. Jemadari alisimama karibu na mfereji wa bwawa lililoko upande wa juu katika barabara kuu inayoelekea uwanda wa Dobi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wa jeshi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Jemadari wa jeshi akasimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme wa Ashuru alimtuma jemadari mkuu kutoka Lakishi na jeshi kubwa kumwendea mfalme Hezekia. Jemadari alisimama karibu na mfereji wa bwawa lililoko upande wa juu katika barabara kuu inayoelekea uwanda wa Dobi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma Amirijeshi kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Amirijeshi aliposimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu lililojengwa, katika njia iendayo kwenye uwanda wa Dobi,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wa jeshi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Jemadari wa jeshi akasimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri toka Lakishi pamoja na jeshi kubwa kwenda hadi Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Naye akasimama karibu na mfereji wa bwawa la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme wa Ashuru alimtuma jemadari mkuu kutoka Lakishi na jeshi kubwa kumwendea mfalme Hezekia. Jemadari alisimama karibu na mfereji wa bwawa lililoko upande wa juu katika barabara kuu inayoelekea uwanda wa Dobi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme wa Asuri akamtuma mkuu wa askari, atoke Lakisi kwenda Yerusalemu na kikosi kikubwa kwake mfalme Hizikia. Akaja kusimama kwenye mfereji wa ziwa la juu katika barabara iendayo Shambani kwa Dobi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme wa Ashuru akamtuma amiri toka Lakishi hata Yerusalemu, kwa mfalme Hezekia, pamoja na jeshi kubwa. Naye akasimama karibu na mfereji wa birika ya juu, iliyo katika njia kuu ya kuuendea uwanda wa dobi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme wa Asuria alimutuma jemadari kutoka Lakisi na kundi kubwa kumwendea mufalme Hezekia. Jemadari yule alisimama karibu na mufereji wa birika linalokuwa upande wa juu katika barabara kubwa inayoelekea shamba la wafuaji wa nguo.