Isaiah 36:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa mkuu wa ikulu, katibu Shebna, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi, wakamwendea mfalme Hezekia huku mavazi yao yakiwa yameraruliwa, wakamweleza maneno ya mkuu wa matowashi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu, na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa, na kumwambia vile jemadari wa jeshi alivyosema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika tarehe, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule amiri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa mkuu wa ikulu, katibu Shebna, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi, wakamwendea mfalme Hezekia huku mavazi yao yakiwa yameraruliwa, wakamweleza maneno ya mkuu wa matowashi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia kiongozi wa jumba la kifalme, Shebna katibu na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa na kumwambia yale Amirijeshi aliyosema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu, na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa, na kumwambia yale jemadari wa jeshi aliyoyasema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika kumbukumbu, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zikiwa zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule kamanda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa mkuu wa ikulu, katibu Shebna, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi, wakamwendea mfalme Hezekia huku mavazi yao yakiwa yameraruliwa, wakamweleza maneno ya mkuu wa matowashi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Eliakimu, mwana wa Hilikia, aliyekuwa mtunza nyumba ya mfalme, na Sebuna aliyekuwa mwandishi na Yoa, mwana wa Asafu, aliyekuwa mwandishi wa mambo yaliyopasa kukumbukwa wakaja kwa Hizikia wenye nguo zilizoraluliwa, wakamsimulia maneno ya mkuu wa askari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Eliakimu, mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna, mwandishi, na Yoa, mwana wa Asafu mwenye kuandika tarehe, wakaenda kwa Hezekia, na nguo zao zimeraruliwa, wakamwambia Hezekia maneno ya yule amiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa musimamizi wa nyumba ya kifalme, Sebuna aliyekuwa katibu, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi, wakamwendea Hezekia na nguo zenye kupasuliwa, wakamwelezea maneno ya yule jemadari.