Isaiah 36:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Angalia! Sasa unategemea Misri, utete uliovunjika ambao utamchoma mkono yeyote atakayeuegemea. Hivyo ndivyo Farao, mfalme wa Misri alivyo, kwa wote wale wanaomtegemea.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huuchoma na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Angalia! Sasa unategemea Misri, utete uliovunjika ambao utamchoma mkono yeyote atakayeuegemea. Hivyo ndivyo Farao, mfalme wa Misri alivyo, kwa wote wale wanaomtegemea.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huutoboa na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huuchoma na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliovunjika, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Angalia! Sasa unategemea Misri, utete uliovunjika ambao utamchoma mkono yeyote atakayeuegemea. Hivyo ndivyo Farao, mfalme wa Misri alivyo, kwa wote wale wanaomtegemea.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazama! Egemeo lako, unaloliegemea, ni Misri, hilo fimbo la utete unyongekao! Mtu akilikongojea, litamwingia kiganjani, limchome. Ndivyo, Farao, mfalme wa Misri, anavyowawia wote waliomwegemea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Angalia sasa. Unategemea Misri, utete uliovunjika ambao utamuchoma mukono yeyote atakayeuegemea. Hivi ndivyo mufalme wa Misri anavyokuwa kwa wote wale wanaomutegemea.