Isaiah 36:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hata kama mkiniambia, ‘Tunamtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,’ je, si huyohuyo ambaye Hezekia aliziharibu madhabahu zake na kuwaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, ‘Mnapaswa kuabudu mbele ya madhabahu hii?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nawe ukiniambia, “Tunamtumainia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu”: Je, si yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya”?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini ukiniambia, Tunamtumaini Bwana, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hata kama mkiniambia, ‘Tunamtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,’ je, si huyohuyo ambaye Hezekia aliziharibu madhabahu zake na kuwaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, ‘Mnapaswa kuabudu mbele ya madhabahu hii?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ukiniambia, “Tunamtumainia BWANA, Mungu wetu,” si ni yeye ambaye mahali pake pa juu na madhabahu zake Hezekia ameziondoa, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima msujudu mbele ya madhabahu hii”?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nawe kama ukiniambia, “Tunamtumainia bwana Mwenyezi Mungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya”?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ukiniambia, Tunamtumaini BWANA, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hata kama mkiniambia, ‘Tunamtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,’ je, si huyohuyo ambaye Hezekia aliziharibu madhabahu zake na kuwaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, ‘Mnapaswa kuabudu mbele ya madhabahu hii?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukiniambia: Tunamwegemea Bwana Mungu wetu, basi, yeye siye, ambaye Hizikia aliwakataza watu kumtambikia vilimani pake napo penye meza zake za kutambikia, alipowaambia Wayuda na Wayerusalemu: Sharti mmwangukie mbele ya meza hii tu ya kumtambikia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini ukiniambia, Tunamtumaini BWANA, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hata kama mukiniambia ‘Tunamutegemea Yawe, Mungu wetu’, si huyohuyo ambaye Hezekia aliziharibu nafasi zake zote za kuabudu kwenye vilima pamoja na mazabahu zake na kuwaambia watu wa Yuda na Yerusalema: Munapaswa kuabudu mbele ya mazabahu hii ya Yerusalema tu?