Isaiah 37:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, unayeketi katika kiti cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa. Wewe ndiwe uliyeumba mbingu na dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, unayeketi kwenye kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia. Wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, unayeketi katika kiti cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa. Wewe ndiwe uliyeumba mbingu na dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Umeumba mbingu na nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia. Wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, unayeketi katika kiti cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa. Wewe ndiwe uliyeumba mbingu na dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, uyakaliaye Makerubi, wewe ndiwe Mungu peke yako wa nchi zote za kifalme, wewe ndiwe uliyezifanya mbingu na nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, ukaaye juu ya makerubi, wewe, naam, wewe peke yako, ndiwe Mungu wa falme zote za dunia. Wewe ndiwe uliyeziumba mbingu na nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ee Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, unayeikaa katika kiti cha kifalme juu ya makerubi, ni wewe tu unayekuwa Mungu, unayetawala falme zote za ulimwengu. Wewe uliumba dunia na mbingu.