Isaiah 37:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Umewatumia watumishi wako kunidhihaki mimi Bwana; wewe umesema, ‘Kwa magari yangu mengi ya vita, nimekwea vilele vya milima, mpaka kilele cha Lebanoni. Nimeangusha mierezi yake mirefu, na misonobari mizurimizuri. Nimevifikia vilele vyake na ndani ya misitu yake mikubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kupitia kwa wajumbe wako umelundika matukano juu ya Bwana. Nawe umesema, ‘Kwa magari yangu mengi ya vita, nimepanda juu ya vilele vya milima, vilele vya juu sana katika Lebanoni. Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu, misunobari yake iliyo bora sana. Nimefikia sehemu zake zilizoinuka juu sana, misitu yake iliyo mizuri sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umemshutumu Bwana kwa watumishi wako, kwa kuwa umesema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani ya Lebanoni; nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misunobari yake mizuri, nami nitaingia ndani ya mahali pake palipoinuka, palipo mbali sana, msitu wa shamba lake lizaalo sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Umewatumia watumishi wako kunidhihaki mimi Bwana; wewe umesema, ‘Kwa magari yangu mengi ya vita, nimekwea vilele vya milima, mpaka kilele cha Lebanoni. Nimeangusha mierezi yake mirefu, na misonobari mizurimizuri. Nimevifikia vilele vyake na ndani ya misitu yake mikubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kutumia wajumbe wako umelundika matukano juu ya Bwana. Nawe umesema, ‘Kwa magari yangu mengi ya vita, nimekwea kwenye vilele vya milima, kwenye vilele vya juu kabisa vya Lebanoni. Nimeikata mierezi yake iliyo mirefu kuliko yote, misonobari yake iliyo bora sana. Nimefika mahali pake palipoinuka palipo mbali sana, katika msitu wake ulio mzuri kuliko yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kupitia kwa wajumbe wako umelundika matukano juu ya Bwana. Nawe umesema, ‘Kwa magari yangu mengi ya vita, nimepanda juu ya vilele vya milima, vilele vya juu sana katika Lebanoni. Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu, misunobari yake iliyo bora sana. Nimefikia sehemu zake zilizoinuka juu sana, misitu yake iliyo mizuri sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umemshutumu Bwana kwa watumishi wako, kwa kuwa umesema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani ya Lebanoni; nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misonobari yake mizuri, nami nitaingia ndani ya mahali pake palipoinuka, palipo mbali sana, msitu wa shamba lake lizaalo sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Umewatumia watumishi wako kunidhihaki mimi Bwana; wewe umesema, ‘Kwa magari yangu mengi ya vita, nimekwea vilele vya milima, mpaka kilele cha Lebanoni. Nimeangusha mierezi yake mirefu, na misonobari mizurimizuri. Nimevifikia vilele vyake na ndani ya misitu yake mikubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ndiye, uliyembeua vinywani mwa watumishi wako ukisema: Kwa kuwa magari yangu ni mengi, nimepanda milimani juu huko ndani Libanoni, nikaikata miangati yake mirefu na mivinje yake iliyochaguliwa, nikafika kwake huko juu kileleni, msitu unakokuwa kama shamba lake la miti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umemshutumu Bwana kwa watumishi wako, kwa kuwa umesema, Kwa wingi wa magari yangu nimepanda juu ya vilele vya milima, mpaka mahali pa ndani ya Lebanoni; nami nitaikata mierezi yake mirefu, na misunobari yake mizuri, nami nitaingia ndani ya mahali pake palipoinuka, palipo mbali sana, msitu wa shamba lake lizaalo sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umewatuma watumishi wako kumuchekelea Bwana wenu; wewe umesema: Kwa magari yangu mengi ya vita, nimefika juu kwenye vichwa vya milima, mpaka kwenye vichwa vya milima ya Lebanoni. Nimeangusha mierezi yake mirefu, na misunobari mizurimizuri. Nimevifikia vichwa vyake na ndani ya pori zake kubwa.