Isaiah 37:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Je, hujasikia ewe Senakeribu kwamba nilipanga jambo hili tangu zamani? Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani. Nilikuweka uifanye miji yenye ngome kuwa rundo la magofu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Je, hujasikia? Zamani sana niliamuru hili. Siku za kale nilipanga hili; sasa nimelifanya litokee, kwamba umegeuza miji yenye ngome kuwa malundo ya mawe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Hukusikia? Ni mimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale; nikayatimiza sasa, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, ikawe chungu na magofu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Je, hujasikia ewe Senakeribu kwamba nilipanga jambo hili tangu zamani? Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani. Nilikuweka uifanye miji yenye ngome kuwa rundo la magofu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Je, hukusikia? Zamani sana nililisimika. Katika siku za zamani nililipanga, na sasa nimelitimiza, kwamba umeigeuza miji yenye maboma kuwa malundo ya mawe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Je, hujasikia? Zamani sana niliamuru hili. Siku za kale nilipanga hili; sasa nimelifanya litokee, kwamba umegeuza miji yenye ngome kuwa malundo ya mawe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Hukusikia? Ni mimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale; nikayatimiza sasa, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, ibomoke na kuwa rundo la magofu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Je, hujasikia ewe Senakeribu kwamba nilipanga jambo hili tangu zamani? Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani. Nilikuweka uifanye miji yenye ngome kuwa rundo la magofu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Hujasikia kwamba: Niliyoyafanya kale, niliyoyalinganisha siku za mbele, sasa nimeyaleta, yatimie; wewe ukawa wa kutowesha miji yenye maboma, iwe machungu ya mawe na mabomoko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Hukusikia? Ni mimi niliyeyatenda hayo tokea zamani, na kuyafanya tokea siku za kale; nikayatimiza sasa, iwe kazi yako kuangamiza miji yenye boma, ikawe chungu na magofu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haujasikia, ewe Saniharibu, kwamba mimi Yawe nilipanga jambo hili tangu zamani? Ninachotimiza sasa nilikipanga zamani. Nilikuweka uifanye miji yenye kuzungukwa na kuta kuwa lundo la mabomoko.