Isaiah 37:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika. Wamekuwa kama mimea shambani, kama nyasi changa shambani, kama majani yaotayo juu ya paa au kama ngano kabla hazijakomaa ambazo hunyauka upepo mkavu uvumapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu, wanavunjika mioyo na kuaibishwa. Wao ni kama mimea katika shamba, kama machipukizi mororo ya kijani, kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, ambayo hukauka kabla ya kukua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndiyo sababu wenyeji wao wakawa hawana nguvu, na kufadhaika, na kuhangaika, wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, kama shamba la ngano kabla haijaiva.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika. Wamekuwa kama mimea shambani, kama nyasi changa shambani, kama majani yaotayo juu ya paa au kama ngano kabla hazijakomaa ambazo hunyauka upepo mkavu uvumapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa miji hiyo, wakiwa wameishiwa nguvu, wanatiwa hofu na kuaibishwa. Wao ni kama mimea katika shamba, kama machipukizi mororo ya kijani, kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, ambayo hukauka kabla ya kukua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu, wanavunjika mioyo na kuaibishwa. Wao ni kama mimea katika shamba, kama machipukizi mororo ya kijani, kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba, ambayo hukauka kabla ya kukua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndiyo sababu wenyeji wao wakawa hawana nguvu, na kufadhaika, na kuhangaika, wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya madari, kama shamba la ngano kabla haijaiva.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufadhaika. Wamekuwa kama mimea shambani, kama nyasi changa shambani, kama majani yaotayo juu ya paa au kama ngano kabla hazijakomaa ambazo hunyauka upepo mkavu uvumapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao waliokaa humo mikono yao ikawa mifupi, wakastuka, wakaingiwa na soni, wakawa kama mapalizi ya shambani au kama ndago za uwandani au kama majani yameayo juu ya kipaa au kama shamba linyaukalo pasipo kuzaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndiyo sababu wenyeji wao wakawa hawana nguvu, na kufadhaika, na kuhangaika, wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, kama shamba la ngano kabla haijaiva.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaaji wake wakiwa wameishiwa nguvu, wametishika na kufazaika, wamekuwa kama mimea ya shamba, kama majani changa, kama majani yanayoota juu ya paa, yanayokauka mbele ya kukomaa.