Isaiah 37:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa vile umefanya mipango dhidi yangu na nimeusikia ufidhuli wako, nitatia ndoana yangu puani mwako, na lijamu yangu kinywani mwako. Nitakurudisha njia ileile uliyojia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu unaghadhibika na ufidhuli dhidi yangu, na kwa sababu ufidhuli wako umefika masikioni mwangu, nitaweka ndoana yangu puani mwako na hatamu yangu kinywani mwako, nami nitakufanya urudi kwa njia ile uliyoijia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu, nitatia kulabu yangu katika pua yako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha kwa njia ile ile uliyoijia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa vile umefanya mipango dhidi yangu na nimeusikia ufidhuli wako, nitatia ndoana yangu puani mwako, na lijamu yangu kinywani mwako. Nitakurudisha njia ileile uliyojia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu unaghadhibika na ufedhuli dhidi yangu na kwa sababu ufidhuli wako umefika masikioni mwangu, nitaweka ndoana yangu kwenye pua yako na hatamu yangu kinywani mwako, nami nitakufanya urudi kwa njia uliyoijia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu unaghadhibika na ufidhuli dhidi yangu, na kwa sababu ufidhuli wako umefika masikioni mwangu, nitaweka ndoana yangu puani mwako na hatamu yangu kinywani mwako, nami nitakufanya urudi kwa njia ile uliyoijia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu, nitatia kulabu yangu katika pua yako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha kwa njia ile ile uliyoijia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa vile umefanya mipango dhidi yangu na nimeusikia ufidhuli wako, nitatia ndoana yangu puani mwako, na lijamu yangu kinywani mwako. Nitakurudisha njia ileile uliyojia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu unanikasirikia, majivuno yako yakapanda kuingia masikioni mwangu, nitakutia pete yangu puani mwako, nayo hatamu yangu midomoni mwako, kisha nitakurudisha katika njia ileile, uliyokuja nayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu, nitatia kulabu yangu katika pua yako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha kwa njia ile ile uliyoijia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa vile umefanya mipango juu yangu na nimesikia majivuno yako, nitatia ndoana yangu ndani ya pua yako, na lijamu yangu ndani ya kinywa chako. Nitakurudisha katika njia ileile uliyokuja ndani yake.