Isaiah 37:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao wakamwambia Isaya, “Hezekia anasema hivi, ‘Leo ni siku ya huzuni, siku ya kukemewa, na ya dharau. Sisi tumekuwa kama mama anayetaka kujifungua mtoto, lakini hana nguvu ya kumzaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wa tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao wakamwambia Isaya, “Hezekia anasema hivi, ‘Leo ni siku ya huzuni, siku ya kukemewa, na ya dharau. Sisi tumekuwa kama mama anayetaka kujifungua mtoto, lakini hana nguvu ya kumzaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama vile wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wako tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao wakamwambia Isaya, “Hezekia anasema hivi, ‘Leo ni siku ya huzuni, siku ya kukemewa, na ya dharau. Sisi tumekuwa kama mama anayetaka kujifungua mtoto, lakini hana nguvu ya kumzaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamwambia: Hivi ndivyo, Hizikia anavyosema: Siku hii ya leo ni siku ya kusongwa na ya kupatilizwa na ya kutupwa, kwani watoto wamefikisha kuzaliwa, lakini nguvu za kuwazaa haziko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwambia, Hezekia asema hivi, Siku hii ni siku ya dhiki, na aibu, na matukano; maana watoto wa tayari kuzaliwa, wala hapana nguvu za kuwazaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakamwambia Isaya: “Hezekia anasema hivi: Leo ni siku ya huzuni, ya kuazibiwa, na ya kuzarauliwa. Sisi tumekuwa kama mwanamuke anayetaka kuzaa mutoto, lakini hana nguvu ya kumuzaa.