Isaiah 37:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakati wa usiku malaika wa Mwenyezi-Mungu aliingia kambini mwa Waashuru na kuwaua watu 185,000. Halafu kulipopambazuka watu hao wote walionekana wakiwa maiti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo malaika wa Mwenyezi Mungu akaenda, akawaua wanajeshi elfu mia moja na themanini na tano katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi malaika wa Bwana alitoka, akaua watu mia na themanini na tano elfu katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakati wa usiku malaika wa Mwenyezi-Mungu aliingia kambini mwa Waashuru na kuwaua watu 185,000. Halafu kulipopambazuka watu hao wote walionekana wakiwa maiti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo malaika wa BWANA akaondoka na kuwaua watu mia themanini na tano elfu katika kambi ya Waashuru. Watu walipoamka asubuhi yake, wote huko walikuwa maiti!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo malaika wa bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakati wa usiku malaika wa Mwenyezi-Mungu aliingia kambini mwa Waashuru na kuwaua watu 185,000. Halafu kulipopambazuka watu hao wote walionekana wakiwa maiti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatokea malaika wa Bwana, akapiga makambini kwa Waasuri watu 185000. Walipoamka asubuhi wakawaona hao wote, ya kuwa wamekufa, ni mizoga tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu mia na themanini na tano elfu katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, malaika wa Yawe aliingia ndani ya kambi ya Waasuria na kuwaua watu elfu mia moja makumi nane na watano. Kesho yake, wakati watu walipoamuka, waliona yale maiti yote.