Isaiah 37:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inawezekana kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alisikia maneno ya mkuu wa matowashi ambaye ametumwa na mfalme wa Ashuru, bwana wake, ili kumtukana Mungu aliye hai, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako atapinga maneno aliyoyasikia; kwa hiyo waombee watu waliobaki.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yamkini Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yamkini Bwana, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo amiri ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na Bwana, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inawezekana kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alisikia maneno ya mkuu wa matowashi ambaye ametumwa na mfalme wa Ashuru, bwana wake, ili kumtukana Mungu aliye hai, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako atapinga maneno aliyoyasikia; kwa hiyo waombee watu waliobaki.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yamkini BWANA, Mungu wako atayasikia maneno ya Amirijeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo BWANA, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako hai.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yamkini bwana, Mungu wako atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayo bwana, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo kamanda ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na BWANA, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inawezekana kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wako alisikia maneno ya mkuu wa matowashi ambaye ametumwa na mfalme wa Ashuru, bwana wake, ili kumtukana Mungu aliye hai, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako atapinga maneno aliyoyasikia; kwa hiyo waombee watu waliobaki.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Labda Bwana Mungu wako ameyasikia yale maneno ya mkuu wa askari, ambayo bwana wake, mfalme wa Asuri, alimtuma kumbeua Mungu Mwenye uzima kwa kuyasema; Bwana Mungu wako na ampatilizie yale maneno, aliyoyasikia! Nawe na uje kuwaombea waliosalia walioko bado!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yamkini BWANA, Mungu wako, atayasikia maneno ya huyo amiri ambaye mfalme wa Ashuru, bwana wake, amemtuma ili amtukane Mungu aliye hai; na BWANA, Mungu wako atayakemea maneno aliyoyasikia; basi, inua dua yako kwa ajili ya mabaki yaliyobakia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Labda Yawe, Mungu wako, alisikia maneno ya yule jemadari ambaye ametumwa na bwana wake mufalme wa Asuria, kwa kumutukana Mungu Mwenye Uzima, naye Yawe, Mungu wako atamwazibu kwa ajili ya maneno aliyoyasikia. Uwaombee watu wanaobaki.”