Isaiah 37:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha yule mkuu wa matowashi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru alikuwa ameondoka Lakishi, aliondoka na kumkuta akishambulia mji wa Libna.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi, akamkuta mfalme akipigana na Libna.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yule amiri akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru anafanya vita juu ya Libna; kwa maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha yule mkuu wa matowashi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru alikuwa ameondoka Lakishi, aliondoka na kumkuta akishambulia mji wa Libna.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amirijeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi akamkuta mfalme anapigana dhidi ya Libna.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi, akamkuta mfalme akipigana na Libna.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yule kamanda akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru anapigana vita juu ya Libna; kwa maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha yule mkuu wa matowashi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru alikuwa ameondoka Lakishi, aliondoka na kumkuta akishambulia mji wa Libna.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkuu wa askari aliporudi akamkuta mfalme wa Asuri, akipiga vita Libuna, kwani alisikia, ya kuwa mfalme ameondoka Lakisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yule amiri akarudi, akamkuta mfalme wa Ashuru anafanya vita juu ya Libna; kwa maana alikuwa amesikia ya kwamba ameondoka, akaacha Lakishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha yule jemadari aliposikia kwamba mufalme wa Asuria alikuwa ameondoka Lakisi, aliondoka na kumukuta akishambulia muji wa Libuna.