Isaiah 38:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, mfalme Hezekia aliugua sana karibu kufa. Ndipo nabii Isaya mwana wa Amozi, akamwendea, akamwambia, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu: Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa kuwa utakufa, hutapona.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, mfalme Hezekia aliugua sana karibu kufa. Ndipo nabii Isaya mwana wa Amozi, akamwendea, akamwambia, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu: Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa kuwa utakufa, hutapona.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hizo Hezekia akaugua naye akawa karibu na kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akamwendea na kumwambia, “Hili ndilo asemalo BWANA: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku hizo Hezekia aliugua, akawa karibu kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, mfalme Hezekia aliugua sana karibu kufa. Ndipo nabii Isaya mwana wa Amozi, akamwendea, akamwambia, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu: Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa kuwa utakufa, hutapona.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile Hizikia akaugua, kufa kukamjia karibu. Ndipo, mfumbuaji Yesaya, mwana wa Amosi, alipokuja kwake, akamwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Yaliyo yako yaagizie walio wa mlango wako! Kwani wewe utakufa, hutarudi kuwa mzima tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, Hezekia aligonjwa sana karibu kufa. Halafu nabii Isaya mwana wa Amozi akamwendea, akamwambia: Yawe anasema hivi: Panga mambo yako sawasawa katika nyumba yako kwa sababu utakufa, hautapona.