Isaiah 38:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hezekia akauliza, “Ni ishara gani itakayonijulisha kwamba mimi nitakwenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu?” Isaya akamjibu, “Hii itakuwa ishara kwako kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwamba Mwenyezi-Mungu atafanya kama alivyoahidi. Nitafanya kivuli kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi, kirudi nyuma hatua kumi.” Nacho kivuli kikarudi nyuma hatua kumi. Kisha mfalme Hezekia alipopona, akatunga wimbo huu wa shukrani: “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa, inanibidi niage dunia. Mimi nimepangiwa kwenda kuzimu siku zote zilizonibakia. Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu, katika nchi ya walio hai; wala sitamwona mtu yeyote tena, miongoni mwa wakazi wa ulimwengu. Makao yangu yamengolewa kwangu, kama hema la mchungaji; kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu; Mungu amenikatilia mbali; kabla hata mwisho wa siku amenikomesha. Usiku kucha nililia kuomba msaada; kama simba, anavunjavunja mifupa yangu; mchana na usiku ananikomesha. “Ninalia kama mbayuwayu, nasononeka kama njiwa. Macho yangu yamefifia kwa kuangalia juu. Ee Bwana, nateseka; uwe wewe usalama wangu! Lakini niseme nini: Yeye mwenyewe aliniambia, naye mwenyewe ametenda hayo. Usingizi wangu wote umenitoroka kwa sababu ya uchungu moyoni mwangu. “Ee Bwana, Sisi twaishi kutokana na yote uliyotenda, kwa hayo yote mimi binafsi pia ninaishi. Nirudishie afya, uniwezeshe kuishi. Nilipata mateso makali kwa faida yangu; lakini umeyaokoa maisha yangu kutoka shimo la uharibifu, maana umezitupa dhambi zangu nyuma yako. Huko kuzimu mtu hawezi kukushukuru wewe; waliokufa hawawezi kukushukuru wewe. Wala washukao huko shimoni hawawezi tena kutumainia uaminifu wako. Walio hai ndio wanaokushukuru, kama na mimi ninavyofanya leo. Kina baba huwajulisha watoto wao uaminifu wako. “Mwenyezi-Mungu ataniokoa. Nasi tutamsifu kwa nyimbo za vinubi siku zote za maisha yetu, nyumbani kwake Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia alikuwa ameuliza, “Kutakuwa na ishara gani kwamba nitapanda kwenda Hekalu la Mwenyezi Mungu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionyesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa Bwana?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hezekia akauliza, “Ni ishara gani itakayonijulisha kwamba mimi nitakwenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia alikuwa ameuliza, “Ni ishara ipi kwamba nitapanda kwenda hekaluni mwa BWANA?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia alikuwa ameuliza, “Kutakuwa na ishara gani kwamba nitapanda kwenda Hekalu la bwana?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa BWANA?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hezekia akauliza, “Ni ishara gani itakayonijulisha kwamba mimi nitakwenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizikia akasema: Kielekezo ni nini cha kwamba: Nitapanda tena kwenda nyumbani mwa Bwana?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionyesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa BWANA?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hezekia akauliza: Ni kitambulisho gani kitakachonijulisha kwamba mimi nitakwenda kwa nyumba ya Yawe?