Isaiah 39:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, mfalme Merodak-baladani mwana wa Baladani, mfalme wa Babuloni, aliposikia kwamba Hezekia alikuwa ameugua na sasa amepona, alimtumia ujumbe pamoja na zawadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani mfalme wa Babeli, akamtumia Hezekia barua na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua na kupona kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati huo Merodaki-baladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana amepata habari kwamba amekuwa hawezi, na kwamba amepona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, mfalme Merodak-baladani mwana wa Baladani, mfalme wa Babuloni, aliposikia kwamba Hezekia alikuwa ameugua na sasa amepona, alimtumia ujumbe pamoja na zawadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo Merodaki-Baladani mwana wa Baladani mfalme wa Babeli alimpelekea Hezekia barua na zawadi, kwa kuwa alikuwa amesikia habari za kuugua na kupona kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani mfalme wa Babeli, akamtumia Hezekia barua na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua na kupona kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati huo Merodak-baladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana amepata habari kwamba amekuwa mgonjwa, na kwamba amepona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, mfalme Merodak-baladani mwana wa Baladani, mfalme wa Babuloni, aliposikia kwamba Hezekia alikuwa ameugua na sasa amepona, alimtumia ujumbe pamoja na zawadi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, akatuma barua na matunzo kwake Hizikia kwani alisikia ya kuwa aliugua, akapona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati huo Merodaki-baladani, mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, alipeleka barua na zawadi kwa Hezekia; kwa maana amepata habari kwamba amekuwa hawezi, na kwamba amepona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo, mufalme Merodaki-Baladani mwana wa Baladani, mufalme wa Babeli, aliposikia kwamba Hezekia alikuwa mugonjwa na sasa amepona, alimutumia wajumbe waliomupelekea barua pamoja na zawadi.