Isaiah 39:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Hezekia aliwakaribisha na kuwaonesha nyumba ya hazina: Fedha, dhahabu, viungo vya kukolezea chakula, mafuta ya thamani, vifaa vyake vyote vya kijeshi na vitu vyote vilivyokuwamo katika bohari zake. Hakuna chochote katika ikulu yake au katika nchi yake ambacho hakuwaonesha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia akawapokea wale wajumbe kwa furaha na kuwaonesha vitu vile vilivyokuwa katika ghala zake: yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha lote, na kila kitu kilichokuwa katika hazina yake. Hapakuwa na kitu katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonesha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hezekia akawafurahia, akawaonyesha nyumba yake yenye vitu vyake vya thamani, fedha na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yote yenye silaha zake za vita, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake; hapakuwa na kitu nyumbani mwake wala katika ufalme wake asichowaonyesha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Hezekia aliwakaribisha na kuwaonesha nyumba ya hazina: fedha, dhahabu, viungo vya kukolezea chakula, mafuta ya thamani, vifaa vyake vyote vya kijeshi na vitu vyote vilivyokuwamo katika bohari zake. Hakuna chochote katika ikulu yake au katika nchi yake ambacho hakuwaonesha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia akawapokea wajumbe hao kwa furaha na kuwaonyesha kile kilichokuwa ndani ya ghala zake: Fedha, dhahabu, vikolezo, mafuta safi, silaha zake zote za vita na kila kitu kilichopo katika hazina zake. Hapakuwepo kitu cho chote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia akawapokea wale wajumbe kwa furaha na kuwaonyesha vitu vile vilivyokuwa katika ghala zake: yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha lote, na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu chochote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia akawafurahia, akawaonesha nyumba yake yenye vitu vyake vya thamani, fedha na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yote yenye silaha zake za vita, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake; hapakuwa na kitu nyumbani mwake wala katika ufalme wake ambacho hakuwaonesha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Hezekia aliwakaribisha na kuwaonesha nyumba ya hazina: Fedha, dhahabu, viungo vya kukolezea chakula, mafuta ya thamani, vifaa vyake vyote vya kijeshi na vitu vyote vilivyokuwamo katika bohari zake. Hakuna chochote katika ikulu yake au katika nchi yake ambacho hakuwaonesha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizikia akawafurahia, akawaonyesha nyumba ya kuwekea mali zake, mlimo na fedha na dhahabu na manukato na mafuta mazuri, nayo nyumba yote ya mata yake, nayo yote pia yaliyooneka katika vilimbiko vyake. Hakikuwako kitu, ambacho Hizikia hakuwaonyesha, wala nyumbani mwake, wala katika ufalme wake wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hezekia akawafurahia, akawaonyesha nyumba yake yenye vitu vyake vya thamani, fedha na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yote yenye silaha zake za vita, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake; hapakuwa na kitu nyumbani mwake wala katika ufalme wake asichowaonyesha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Hezekia aliwakaribisha na kuwaonyesha nyumba alimoweka mali yake: feza, zahabu, viungo vya kukoleza chakula, mafuta ya bei kali, vifaa vyake vyote vya vita na vitu vyote vilivyokuwa katika gala zake. Hakuna chochote katika nyumba yake ya kifalme au katika inchi yake ambacho hakuwaonyesha.