Isaiah 39:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena baadhi ya watoto wako mwenyewe wa kiume watapelekwa mateka nao watakuwa matowashi katika ikulu ya mfalme wa Babuloni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao baadhi ya wazao wako, mwili wako na damu yako mwenyewe watakaozaliwa kwako, watachukuliwa mbali, nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na baadhi ya wana wako utakaowazaa, watakaotoka kwako, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena baadhi ya watoto wako mwenyewe wa kiume watapelekwa mateka nao watakuwa matowashi katika ikulu ya mfalme wa Babuloni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tena baadhi ya wazao wako, watu wa nyama na damu yako mwenyewe watakaozaliwa kwako, watachukuliwa, nao watakuwa matowashi katika jumba la kifalme la mfalme wa Babeli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao baadhi ya wazao wako, nyama yako na damu yako mwenyewe watakaozaliwa kwako, watachukuliwa mbali, nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na baadhi ya wana wako utakaowazaa, watakaotoka kwako, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena baadhi ya watoto wako mwenyewe wa kiume watapelekwa mateka nao watakuwa matowashi katika ikulu ya mfalme wa Babuloni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo katika wanao wa kiume waliotoka mwilini mwako, uliowazaa mwenyewe, watachukuliwa wengine, watumikie jumbani mwa mfalme wa Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na baadhi ya wana wako utakaowazaa, watakaotoka kwako, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena wamoja kati ya watoto wako wanaume watapelekwa, nao watakuwa matowashi watakaotumika katika nyumba ya mufalme wa Babeli.