Isaiah 4:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ile, tawi atakalochipusha Mwenyezi-Mungu litakuwa zuri na tukufu, nayo matunda ya nchi yatakuwa ya fahari na utukufu kwa wale Waisraeli watakaosalia. Waisraeli watakaobaki watayaonea fahari na kujivunia mazao ya nchi yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ile Tawi la Mwenyezi Mungu litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ile, tawi atakalochipusha Mwenyezi-Mungu litakuwa zuri na tukufu, nayo matunda ya nchi yatakuwa ya fahari na utukufu kwa wale Waisraeli watakaosalia. Waisraeli watakaobaki watayaonea fahari na kujivunia mazao ya nchi yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ile Tawi la BWANA litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ile Tawi la bwana litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ile, tawi atakalochipusha Mwenyezi-Mungu litakuwa zuri na tukufu, nayo matunda ya nchi yatakuwa ya fahari na utukufu kwa wale Waisraeli watakaosalia. Waisraeli watakaobaki watayaonea fahari na kujivunia mazao ya nchi yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile mche wa Bwana utakuwa wenye urembo na macheo, nao uzao wa nchi utakuwa wenye ukuu na utukufu kwao Waisiraeli waliopona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ile, tawi Yawe atakalochipuza litakuwa zuri na tukufu, nayo matunda ya inchi yatakuwa na heshima na utukufu kwa wale Waisraeli watakaobaki. Waisraeli watakaobaki watasifiwa na kujivunia mazao ya inchi yao.