Isaiah 4:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
hapo atafanya kila mahali juu ya mlima Siyoni na juu ya mikutano ya watu kuwe na wingu wakati wa mchana, na moshi na moto uwakao vizuri wakati wa usiku. Zaidi ya hayo utukufu wa Mungu utaufunika na kuulinda mji wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Mwenyezi Mungu ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni, na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana, na kung’aa kwa miali ya moto wakati wa usiku; nako juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, Bwana ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
hapo atafanya kila mahali juu ya mlima Siyoni na juu ya mikutano ya watu kuwe na wingu wakati wa mchana, na moshi na moto uwakao vizuri wakati wa usiku. Zaidi ya hayo utukufu wa Mungu utaufunika na kuulinda mji wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha BWANA ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana na kung'aa kwa miali ya moto wakati wa usiku, juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha bwana ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni, na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana, na kung’aa kwa miali ya moto wakati wa usiku, nako juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, BWANA ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
hapo atafanya kila mahali juu ya mlima Siyoni na juu ya mikutano ya watu kuwe na wingu wakati wa mchana, na moshi na moto uwakao vizuri wakati wa usiku. Zaidi ya hayo utukufu wa Mungu utaufunika na kuulinda mji wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwenye makao yote ya mlimani kwa Sioni nako kwenye makutano ya kumtambikia Bwana atakuumbia siku zote wingu litakalokuwa lenye moshi la mchana na lenye mwanga wa moto uwakao usiku, kwani chote chenye utukufu hupaswa na kifuniko chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, BWANA ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, kila pahali juu ya mulima Sayuni na juu ya mikutano ya watu atafanya kuwe wingu wakati wa muchana, na moshi na moto unaowaka vizuri wakati wa usiku. Zaidi ya hayo utukufu wa Mungu utaufunika na kuulinda muji wote.