Isaiah 40:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, ni kama vumbi juu ya mizani. Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo, ni kama vumbi jembamba juu ya mizani, huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, ni kama vumbi juu ya mizani. Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo, ni kama vumbi jembamba juu ya mizani, huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo, ni kama vumbi jembamba juu ya mizani, huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, ni kama vumbi juu ya mizani. Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni: mataifa mazima huwaziwa kuwa kama tone la maji katika ndoo, au kama kivumbi katika mizani! Tazameni: visiwa ni kama kichanga alichokiokota!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visiwa kama ni kitu kidogo sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwake mataifa ni kama tone la maji katika mbeketi, ni kama mavumbi juu ya kilo. Kwake visanga ni vyepesi kama mavumbi laini.