Isaiah 40:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Au ni sanamu ya mti mgumu? Hiyo ni ukuni mtu anaochagua, akamtafuta fundi stadi, naye akamchongea sanamu imara!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii huuchagua mti usiooza. Humtafuta fundi stadi wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi mstadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Au ni sanamu ya mti mgumu? Hiyo ni ukuni mtu anaochagua, akamtafuta fundi stadi, naye akamchongea sanamu imara!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii huuchagua mti usiooza. Humtafuta fundi stadi wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii huuchagua mti usiooza. Humtafuta fundi stadi wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi stadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Au ni sanamu ya mti mgumu? Hiyo ni ukuni mtu anaochagua, akamtafuta fundi stadi, naye akamchongea sanamu imara!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akosaye mali za kununua kipaji kama hicho huchagua mti usiooza, kisha hutafuta fundi aijuaye kazi hiyo, amsimamishie kinyago kisichoyumbayumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye aliye maskini sana hata hawezi kutoa sadaka ya namna hii, huchagua mti usiooza, hujitafutia fundi mstadi wa kusimamisha sanamu ya kuchonga isiyoweza kutikisika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Au ni sanamu ya muti mugumu? Hiyo ni kuni mutu anayochagua, akamutafuta fundi anayeelewa kazi, naye anamuchongea sanamu imara!