Isaiah 41:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nimechochea mtu toka kaskazini, naye amekuja; naam, nimemchagua mtu toka mashariki, naye atalitamka jina langu. Yeye atawakanyaga wafalme kama tope, kama vile mfinyanzi apondavyo udongo wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini, naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu. Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye amekuja; toka maawio ya jua amekuja anitajaye jina langu; naye atawajilia maliwali kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi afinyangaye udongo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nimechochea mtu toka kaskazini, naye amekuja; naam, nimemchagua mtu toka mashariki, naye atalitamka jina langu. Yeye atawakanyaga wafalme kama tope, kama vile mfinyanzi apondavyo udongo wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini, naye yuaja, mmoja toka maawio ya jua aliitaye Jina langu. Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini, naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu. Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye amekuja; toka mawio ya jua amekuja anitajaye jina langu; naye atawakanyaga watawala kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi apondaye udongo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nimechochea mtu toka kaskazini, naye amekuja; naam, nimemchagua mtu toka mashariki, naye atalitamka jina langu. Yeye atawakanyaga wafalme kama tope, kama vile mfinyanzi apondavyo udongo wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nimeamsha mtu upande wa kaskazini, akaja; nimemtoa maawioni kwa jua atakayelitambikia Jina langu. Akawajia wakuu na kuwawazia kuwa mchanga, awaponde, kama mfinyanzi anavyoponda udongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nimemwinua mtu toka kaskazini, naye amekuja; toka maawio ya jua amekuja anitajaye jina langu; naye atawajilia maliwali kama akanyagaye matope, na kama mfinyanzi afinyangaye udongo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimetokeza mutu toka kaskazini, naye amekuja; nimemuchagua mutu toka mashariki, naye atalitaja jina langu. Yeye atawakanyaga wafalme kama matope, kama vile mufinyanzi anavyoponda udongo wake.