Isaiah 41:26 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nani aliyebashiri haya tangu mwanzo, hata sisi tupate kuyatambua? Nani aliyetangulia kuyatangaza, ili sasa tuseme, alisema ukweli? Hakuna hata mmoja wenu aliyeyataja, wala hakuna aliyesikia maneno yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua, au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa mwenye haki’? Hakuna aliyenena hili, hakuna aliyetangulia kusema hili, hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; naam, hapana hata mmoja aliyetuonyesha; naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nani aliyebashiri haya tangu mwanzo, hata sisi tupate kuyatambua? Nani aliyetangulia kuyatangaza, ili sasa tuseme, alisema ukweli? Hakuna hata mmoja wenu aliyeyataja, wala hakuna aliyesikia maneno yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua, au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’? Hakuna aliyenena hili, hakuna aliyetangulia kusema hili, hakuna ye yote aliyesikia maneno kutoka kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua, au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’? Hakuna aliyenena hili, hakuna aliyetangulia kusema hili, hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; naam, hapana hata mmoja aliyetuonesha; naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nani aliyebashiri haya tangu mwanzo, hata sisi tupate kuyatambua? Nani aliyetangulia kuyatangaza, ili sasa tuseme, alisema ukweli? Hakuna hata mmoja wenu aliyeyataja, wala hakuna aliyesikia maneno yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yuko nani aliyeyaagua tangu mwanzo, tukayajua? Yuko nani aliyeyasema kale, tukayaitikia kwamba: Amesema kweli? Lakini hakuna aliyeyaagua, kweli hakuna aliyeyatangaza, wala hakuna aliyeyasikia maneno yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani aliyeihubiri habari tokea mwanzo, tupate kuijua? Na tokea zamani, tupate kusema, Yeye ni mwenye haki? Naam, hapana hata mmoja aliyetujulisha; naam, hapana hata mmoja aliyetuonyesha; naam, hapana hata mmoja aliyesikia maneno yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nani aliyetangaza haya tangu mwanzo, hata sisi tupate kuyatambua? Nani aliyetangulia kuyatangaza, kusudi sasa tuseme, alisema ukweli? Hakuna hata mumoja kati yenu aliyeyataja, wala hakuna aliyesikia maneno yenu.