Isaiah 42:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza; mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye. Nimeiweka roho yangu juu yake, naye atayaletea mataifa haki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, mteule wangu, ninayependezwa naye; nitaweka Roho yangu juu yake, naye ataleta haki kwa mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza; mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye. Nimeiweka roho yangu juu yake, naye atayaletea mataifa haki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye; nitaweka Roho yangu juu yake, naye ataleta haki kwa mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Huyu hapa mtumishi wangu, ninayemtegemeza, mteule wangu, ambaye ninapendezwa naye; nitaweka Roho yangu juu yake, naye ataleta haki kwa mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza; mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye. Nimeiweka roho yangu juu yake, naye atayaletea mataifa haki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtazameni mtumishi wangu, nimshikizaye! Mtazameni mteule wangu, ambaye Roho yangu inapendezwa naye! Nitamtia Roho yangu, awatolee wamizimu habari, ya kwamba hukumu yao iko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muangalie mutumishi wangu ninayemusaidia; muchaguliwa wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye. Nimeiweka roho yangu juu yake, naye ataimarisha sheria yangu katika mataifa.