Isaiah 42:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, na Israeli kwa wateka nyara? Je, hakuwa yeye, Mwenyezi Mungu, ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? Kwa kuwa hawakufuata njia zake, hawakutii sheria zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, Bwana? Yeye tuliyemkosa, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao? Nani aliyewaacha wanyang'anywe mali zao? Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, na Israeli kwa wateka nyara? Je, hakuwa BWANA, ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? Kwa kuwa hawakufuata njia zake, hawakutii sheria zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka, na Israeli kwa wateka nyara? Je, hakuwa yeye, bwana, ambaye tumetenda dhambi dhidi yake? Kwa kuwa hawakufuata njia zake, hawakutii sheria zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang'anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosea, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni nani aliyemtoa Yakobo, apokonywe mali zake? Ni nani aliyemtia Isiraeli mikononi mwa wanyang'anyi? Si mimi Bwana, waliyemkosea, walipokataa kuzishika njia zangu na kuyasikia Maonyo yangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni nani aliyemtoa Yakobo awe mateka, aliyemtia Israeli katika mikono ya wanyang’anyi? Si yeye, BWANA? Yeye tuliyemkosa, ambaye hawakutaka kwenda katika njia zake, wala hawakuitii sheria yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni nani aliyewatia Waisraeli katika mikono ya waadui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Yawe ambaye tumemukosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake.