Isaiah 43:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hamjaniletea kondoo wenu wa sadaka za kuteketezwa, wala kuniheshimu kwa tambiko zenu. Nami sikuwalemeza kwa kutaka sadaka, wala sikuwachosha kwa kuwadai ubani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala kuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukulemea kwa sadaka za nafaka wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hamjaniletea kondoo wenu wa sadaka za kuteketezwa, wala kuniheshimu kwa tambiko zenu. Nami sikuwalemeza kwa kutaka sadaka, wala sikuwachosha kwa kuwadai ubani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala kuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukulemea kwa sadaka za nafaka wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala kuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukulemea kwa sadaka za nafaka wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hamjaniletea kondoo wenu wa sadaka za kuteketezwa, wala kuniheshimu kwa tambiko zenu. Nami sikuwalemeza kwa kutaka sadaka, wala sikuwachosha kwa kuwadai ubani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hukuniletea wana kondoo wako kuwa wa kunitambikia, wala hukuniheshimu na kunitolea vipaji vya tambiko. Nami sikukusumbua, unipatie matunzo, wala sikukuchokesha na kutaka uvumba kwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamujaniletea kondoo wenu wa sadaka za kuteketezwa, wala kuniheshimu kwa sadaka zenu. Nami sikuwalemea ninyi kwa kutaka sadaka, wala sikuwachokesha kwa kuwadai ubani.