Isaiah 43:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hamkuninunulia manukato kwa faida yenu, wala kuniridhisha kwa nyama nono za tambiko. Badala yake dhambi zenu zimekuwa mzigo kwangu, mmenichosha kabisa kwa makosa yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hukuninunulia uvumba wowote wenye manukato, wala hukunipa kwa ukarimu mafuta ya wanyama wa dhabihu zako. Lakini umenilemea kwa dhambi zako, na kunitaabisha kwa makosa yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hamkuninunulia manukato kwa faida yenu, wala kuniridhisha kwa nyama nono za tambiko. Badala yake dhambi zenu zimekuwa mzigo kwangu, mmenichosha kabisa kwa makosa yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hukuninunulia uvumba wo wote wenye manukato, wala hukunipa kwa ukarimu mafuta ya wanyama wa dhabihu zako. Lakini umenilemea kwa dhambi zako na kunitaabisha kwa makosa yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hukuninunulia uvumba wowote wenye manukato, wala hukunipa kwa ukarimu mafuta ya wanyama wa dhabihu zako. Lakini umenilemea kwa dhambi zako, na kunitaabisha kwa makosa yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hamkuninunulia manukato kwa faida yenu, wala kuniridhisha kwa nyama nono za tambiko. Badala yake dhambi zenu zimekuwa mzigo kwangu, mmenichosha kabisa kwa makosa yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hukuninunulia vipande vya kichiri na kutoa fedha zako, wala hukuninywesha mafuta ya ng'ombe zako za tambiko. Ila ulinisumbua kwa makosa yako, ukanichokesha kwa manza zako, ulizozikora.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hamukuninunulia marasi kwa mali yenu, wala kunishibisha kwa mafuta za sadaka. Pahali pake zambi zenu zimekuwa muzigo kwangu, mumenichokesha kabisa kwa makosa yenu.