Isaiah 43:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mataifa yote na yakusanyike, watu wote na wakutane pamoja. Nani kati ya miungu yao awezaye kutangaza yatakayotukia? Nani awezaye kutuonesha yanayotukia sasa? Wawalete mashahidi wao kuthibitisha kwamba walifanya hivyo. Waache wasikilize na kusema, “Ilikuwa kweli.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mataifa yote yanakutanika pamoja, na makabila yanakusanyika. Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya, na kututangazia mambo yaliyopita? Walete mashahidi wao ili kuwathibitisha kuwa walikuwa sahihi, ili wengine waweze kusikia, waseme, “Ni kweli.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonyesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mataifa yote na yakusanyike, watu wote na wakutane pamoja. Nani kati ya miungu yao awezaye kutangaza yatakayotukia? Nani awezaye kutuonesha yanayotukia sasa? Wawalete mashahidi wao kuthibitisha kwamba walifanya hivyo. Waache wasikilize na kusema, “Ilikuwa kweli.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mataifa yote yanakutanika pamoja na mataifa wanakusanyika. Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya na kututangazia mambo yaliyopita? Walete mashahidi wao ili kuthibitisha kuwa walikuwa sahihi, ili kwamba wengine waweza kusikia na kusema, “Ni kweli.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mataifa yote yanakutanika pamoja, na makabila yanakusanyika. Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya, na kututangazia mambo yaliyopita? Walete mashahidi wao ili kuwathibitisha kuwa walikuwa sahihi, ili wengine waweze kusikia, waseme, “Ni kweli.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mataifa yote na yakusanyike, watu wote na wakutane pamoja. Nani kati ya miungu yao awezaye kutangaza yatakayotukia? Nani awezaye kutuonesha yanayotukia sasa? Wawalete mashahidi wao kuthibitisha kwamba walifanya hivyo. Waache wasikilize na kusema, “Ilikuwa kweli.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wamizimu wote na wakusanyike pamoja, makabila ya watu na yakutane; kwao yuko nani aliyetangaza kama hayo? Yuko nani aliyetuambia yale ya mbele? Na watoe mashahidi, wapate kushinda shaurini, watu wayasikie, kisha waseme: Ni kweli!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wakusanyike mataifa yote, kabila zote wakutanike; ni nani miongoni mwao awezaye kuhubiri neno hili, na kutuonyesha mambo ya zamani? Na walete mashahidi wao, wapate kuhesabiwa kuwa na haki; au na wasikie, wakaseme, Ni kweli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mataifa yote yakusanyike, watu wote wakutane pamoja. Nani kati ya miungu yao anayeweza kutangaza yatakayotukia? Nani anayeweza kutuonyesha yanayotukia sasa? Wawalete washuhuda wao, kuhakikisha kwamba walifanya hivyo. Uwaache wasikilize na kusema: Ilikuwa kweli.