Isaiah 44:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kadhalika naye seremala hupima kipande cha mbao, akakitia alama kwa kalamu yake, kisha kwa vifaa vyake hukichonga na kukipa umbo la binadamu na sura ya kupendeza; kisha akaiweka sanamu hiyo ya mungu mahali pake pa pekee.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Seremala hupima kwa kutumia kamba, na huuchora mstari kwa kalamu; huchonga kwa patasi na kutia alama kwa bikari. Huitengeneza katika umbo la binadamu, umbo la binadamu katika utukufu wake wote, ili iweze kukaa katika mahali pake pa ibada za sanamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwa mfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kadhalika naye seremala hupima kipande cha mbao, akakitia alama kwa kalamu yake, kisha kwa vifaa vyake hukichonga na kukipa umbo la binadamu na sura ya kupendeza; kisha akaiweka sanamu hiyo ya mungu mahali pake pa pekee.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Seremala hupima kwa kutumia kamba na huuchora mstari kwa kalamu; huchonga kwa patasi na kutia alama kwa bikari. Huifanyiza katika umbo la binadamu, la mwanadamu katika utukufu wake wote, ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Seremala hupima kwa kutumia kamba na huuchora mstari kwa kalamu; huchonga kwa patasi na kutia alama kwa bikari. Huifanyiza katika umbo la binadamu, la mwanadamu katika utukufu wake wote, ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwa mfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kadhalika naye seremala hupima kipande cha mbao, akakitia alama kwa kalamu yake, kisha kwa vifaa vyake hukichonga na kukipa umbo la binadamu na sura ya kupendeza; kisha akaiweka sanamu hiyo ya mungu mahali pake pa pekee.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fundi wa kuchonga miti huipima kwa kamba na kuiandika kwa kalamu; kisha hutumia visu na kupimapima tena penye kuviringana. Hivyo anatengeneza kinyago, kifanane na mtu mwenye utukufu wa kimtu, kikae nyumbani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwa mfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile muchoraji wa miti anafanya vipimo vyake kwa kamba, anachapa kitambulisho chake, kisha anatumia vifaa vyake kwa kuchonga. Halafu anatengeneza sanamu na kuipatia umbo la mutu na sura ya kupendeza; kisha anaweka sanamu hiyo ya mungu pahali pake pa pekee.