Isaiah 44:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu hukata mti wa mwerezi ili autumie, au huchagua mberoshi au mwaloni. Huuacha ukue kati ya miti ya msituni. Au hupanda mwerezi na mvua huustawisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hukata miti ya mierezi, huchukua mtiriza au mwaloni. Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni, au hupanda msunobari, nayo mvua huufanya ukue.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu hukata mti wa mwerezi ili autumie, au huchagua mberoshi au mwaloni. Huuacha ukue kati ya miti ya msituni. Au hupanda mwerezi na mvua huustawisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hukata miti ya mierezi, huchukua mteashuri au mwaloni. Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni, au hupanda msunobari, mvua huufanya ukue.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hukata miti ya mierezi, huchukua mtiriza au mwaloni. Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni, au hupanda msunobari, nayo mvua huufanya ukue.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu hukata mti wa mwerezi ili autumie, au huchagua mberoshi au mwaloni. Huuacha ukue kati ya miti ya msituni. Au hupanda mwerezi na mvua huustawisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huagiza watu, wamkatie miangati, huchukua hata mipingo na mivule, hujichagulia miti ya mwituni iliyo migumu, hupanda nayo mise, mvua iikuze.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu anakata muti wa mwerezi kusudi autumie, au anachagua muvula au mwalo. Anauacha ukomae kati ya miti ya pori. Au anaupanda mwerezi na mvua inaustawisha.