Isaiah 44:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sehemu ya mti huo itatumiwa kama kuni; mtu huota moto wake na kuoka mikate yake juu yake. Sehemu nyingine ya mti huohuo, mtu hujichongea sanamu ya mungu, akainakshi, halafu akaiabudu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni kuni ya binadamu: yeye huchukua baadhi yake na kuota moto, huwasha moto na kuoka mkate. Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu, huitengeneza sanamu na kuisujudia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sehemu ya mti huo itatumiwa kama kuni; mtu huota moto wake na kuoka mikate yake juu yake. Sehemu nyingine ya mti huohuo, mtu hujichongea sanamu ya mungu, akainakshi, halafu akaiabudu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni kuni kwa ajili ya binadamu, huchukua baadhi yake na kuota moto, huwasha moto na kuoka mkate. Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu, huitengeneza sanamu na kuisujudia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni kuni ya binadamu: yeye huchukua baadhi yake na kuota moto, huwasha moto na kuoka mkate. Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu, huitengeneza sanamu na kuisujudia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sehemu ya mti huo itatumiwa kama kuni; mtu huota moto wake na kuoka mikate yake juu yake. Sehemu nyingine ya mti huohuo, mtu hujichongea sanamu ya mungu, akainakshi, halafu akaiabudu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu huitumia ya kuchoma moto, huchukua vibanzi vyao vya kuotea, vingine huvitumia jikoni vya kuchomea mikate, tena kipande hukitengeneza kuwa mungu wa kuuangukia; alipokwisha kufanya kinyago, hukitambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sehemu ya muti huo itatumiwa kama kuni; mutu anaota moto wake na kuchoma mikate yake juu yake. Sehemu nyingine ya muti huohuo, mutu anajichongea mungu na kumwabudu; anajitengenezea sanamu ya mungu na kupiga magoti mbele yake.