Isaiah 44:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi, Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyekufanya tangu tumboni mwa mama yako, nimekuja kukusaidia wewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Usiogope, ewe taifa la Yakobo, mtumishi wangu, naam, usiogope ewe Yeshuruni mteule wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni, yeye atakayekusaidia: Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi, Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyekufanya tangu tumboni mwa mama yako, nimekuja kukusaidia wewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Usiogope, ewe taifa la Yakobo, mtumishi wangu, naam, usiogope ewe Yeshuruni mteule wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA, yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni, yeye atakayekusaidia: Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana, yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni, yeye atakayekusaidia: Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi, Mwenyezi-Mungu Muumba wako, niliyekufanya tangu tumboni mwa mama yako, nimekuja kukusaidia wewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nasema: Usiogope, ewe taifa la Yakobo, mtumishi wangu, naam, usiogope ewe Yeshuruni mteule wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana aliyekuumba, aliyekutengeneza tumboni mwa mama, anayekusaidia: Usiogope, mtumishi wangu Yakobo, nawe Isiraeli uongokaye, niliyemchagua!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi, Yawe Muumba wako, niliyekutengeza tangia tumbo la mama yako, ninakuja kukusaidia wewe. Mimi Yawe ninasema hivi: Musiogope, enyi wazao wa Yakobo, mutumishi wangu, usiogope, ewe Yeshuruni, muchaguliwa wangu.