Isaiah 44:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Imbeni kwa furaha enyi mbingu, kwa sababu ya hayo aliyotenda Mwenyezi-Mungu. Pazeni sauti enyi vilindi vya dunia! Imbeni kwa furaha enyi milima! Enyi misitu na miti yote iliyomo, imbeni. Maana Mwenyezi-Mungu amewakomboa wazawa wa Yakobo, naye atatukuka katika nchi ya Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Enyi mbingu, imbeni kwa furaha, kwa maana Mwenyezi Mungu amefanya jambo hili. Ee vilindi vya dunia, piga kelele. Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo, enyi misitu na miti yenu yote, kwa maana Mwenyezi Mungu amemkomboa Yakobo, ameuonesha utukufu wake katika Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Imbeni, enyi mbingu, maana Bwana ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana Bwana amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Imbeni kwa furaha enyi mbingu, kwa sababu ya hayo aliyotenda Mwenyezi-Mungu. Pazeni sauti enyi vilindi vya dunia! Imbeni kwa furaha enyi milima! Enyi misitu na miti yote iliyomo, imbeni. Maana Mwenyezi-Mungu amewakomboa wazawa wa Yakobo, naye atatukuka katika nchi ya Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Enyi mbingu, imbeni kwa furaha, kwa maana BWANA amefanya jambo hili, Ee vilindi vya dunia, piga kelele. Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo, enyi misitu na miti yenu yote, kwa maana BWANA amemkomboa Yakobo, ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Enyi mbingu, imbeni kwa furaha, kwa maana bwana amefanya jambo hili. Ee vilindi vya dunia, piga kelele. Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo, enyi misitu na miti yenu yote, kwa maana bwana amemkomboa Yakobo, ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Imbeni kwa furaha enyi mbingu, kwa sababu ya hayo aliyotenda Mwenyezi-Mungu. Pazeni sauti enyi vilindi vya dunia! Imbeni kwa furaha enyi milima! Enyi misitu na miti yote iliyomo, imbeni. Maana Mwenyezi-Mungu amewakomboa wazawa wa Yakobo, naye atatukuka katika nchi ya Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Shangilieni, mbingu, ya kuwa Bwana ameyatimiza! Pigeni kelele, vilindi vya kuzimuni! Pigeni shangwe na kupaza sauti, milima na misitu na miti yote iliyomo! Kwani Bwana amemwokoa Yakobo, nako kwake Isiraeli anautokeza utukufu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muimbe kwa furaha enyi mbingu, kwa sababu ya yale Yawe aliyotenda. Mupige kelele enyi vilindi vya dunia! Mupige vigelegele enyi milima! Enyi mapori na miti yote inayokuwa ndani yake, mushangilie. Maana Yawe amewakomboa wazao wa Yakobo, naye atatukuzwa katika inchi ya Israeli.