Isaiah 44:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wako, aliyekuumba tangu tumboni mwa mama yako, asema: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyeumba vitu vyote. Mimi peke yangu nilizitandaza mbingu, niliiumba dunia kwa nguvu yangu mwenyewe!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: “Mimi ni Mwenyezi Mungu, niliyeumba vitu vyote, niliyezitanda mbingu peke yangu, niliyeitandaza nchi mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wako, aliyekuumba tangu tumboni mwa mama yako, asema: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyeumba vitu vyote. Mimi peke yangu nilizitandaza mbingu, niliiumba dunia kwa nguvu yangu mwenyewe!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo asemalo BWANA, Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: “Mimi ni BWANA, yeye aliyeumba vitu vyote, yeye peke yake aliyezitanda mbingu, yeye aliyeitandaza nchi mwenyewe,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo asemalo bwana, Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni: “Mimi ni bwana, niliyeumba vitu vyote, niliyezitanda mbingu peke yangu, niliyeitandaza nchi mwenyewe,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu, Mkombozi wako, aliyekuumba tangu tumboni mwa mama yako, asema: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu niliyeumba vitu vyote. Mimi peke yangu nilizitandaza mbingu, niliiumba dunia kwa nguvu yangu mwenyewe!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, anavyosema Bwana, mkombozi wako, aliyekutengeneza tumboni mwa mama: Mimi Bwana niliyafanya yote. Mimi nilipoziwamba mbingu peke yangu, nikazitanda hata nchi, yuko nani aliyekuwa kwangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mukombozi wako, aliyekuumba tangu katika tumbo, anasema hivi: Mimi ndiye Yawe niliyeumba vitu vyote. Mimi peke yangu nilizitandaza mbingu, niliiumba dunia kwa nguvu yangu mwenyewe!