Isaiah 44:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini huuthibitisha ujumbe wa mtumishi wangu, na kukamilisha maaguzi ya wajumbe wangu. Mimi ndimi niuambiaye mji wa Yerusalemu: Wewe Yerusalemu, utakaliwa tena na watu. Na miji ya Yuda: Nyinyi mtajengeka tena: Magofu yenu nitayarekebisha tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi ndimi niyathibitishaye maneno ya watumishi wake, na kutimiza utabiri wa wajumbe wake. “Mimi ndiye niiambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’ niiambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’ na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini huuthibitisha ujumbe wa mtumishi wangu. na kukamilisha maaguzi ya wajumbe wangu. Mimi ndimi niuambiaye mji wa Yerusalemu: Wewe Yerusalemu, utakaliwa tena na watu. Na miji ya Yuda: Nyinyi mtajengeka tena: magofu yenu nitayarekebisha tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ayathibitishaye maneno ya watumishi wake, na kutimiza utabiri wa wajumbe wake, “yeye aiambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’ aiambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’ na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
niyathibitishaye maneno ya watumishi wake, na kutimiza utabiri wa wajumbe wake, “niambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’ niambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’ na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini huuthibitisha ujumbe wa mtumishi wangu, na kukamilisha maaguzi ya wajumbe wangu. Mimi ndimi niuambiaye mji wa Yerusalemu: Wewe Yerusalemu, utakaliwa tena na watu. Na miji ya Yuda: Nyinyi mtajengeka tena: Magofu yenu nitayarekebisha tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Neno la mtumishi wake hulisimamisha, nayo mashauri ya wajumbe wake huyatimiza. Ni yeye auambiaye Yerusalemu: Na ukaliwe! Nayo miji ya Yuda anaiambia: Jengweni! Nami nitayasimamisha mabomoko yao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninahakikisha ujumbe wa mutumishi wangu, na kukamilisha mipango ya wajumbe wangu. Mimi ndiye ninayesema juu ya Yerusalema: Wewe Yerusalema, watu watakaa ndani yako tena. Na juu ya miji ya Yuda: Ninyi mutajengwa tena: mabomoko yenu yatatengenezwa tena.