Isaiah 44:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote wanaotengeneza sanamu za miungu ni bure kabisa; na vitu hivyo wanavyovifurahia haviwafai chochote. Wanaoshuhudia hiyo miungu ya uongo ni vipofu na wajinga. Kwa hiyo hao wataaibishwa!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wote wachongao sanamu ni ubatili, navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. Wale ambao wanazitetea ni vipofu, ni wajinga, nao waaibika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote wanaotengeneza sanamu za miungu ni bure kabisa; na vitu hivyo wanavyovifurahia haviwafai chochote. Wanaoshuhudia hiyo miungu ya uongo ni vipofu na wajinga. Kwa hiyo hao wataaibishwa!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wote wachongao sanamu ni ubatili, navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. Wale ambao wangesema juu yao ni vipofu, ni wajinga, ili wao waaibike.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wote wachongao sanamu ni ubatili, navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu. Wale ambao wanazitetea ni vipofu, ni wajinga, nao waaibika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote wanaotengeneza sanamu za miungu ni bure kabisa; na vitu hivyo wanavyovifurahia haviwafai chochote. Wanaoshuhudia hiyo miungu ya uongo ni vipofu na wajinga. Kwa hiyo hao wataaibishwa!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watengenezao vinyago wote si kitu, navyo viumbe vyao vya kupendeza havifai, wanaovishuhudia wenyewe hawaoni, wala hawatambui kazi, ambazo vilizifanya, kusudi wapatwe na soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wote wanaotengeneza sanamu za miungu ni bure kabisa; na vitu hivyo wanavyovifurahia haviwafalii kitu chochote. Wanaoshuhudia hiyo miungu ya uongo ni vipofu na wajinga. Kwa hiyo hao watafezeheshwa!