Isaiah 45:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Koreshi: “Wewe ni mfalme wangu niliyekuteua; mimi naitegemeza nguvu yako ili uyashinde mataifa mbele yako, na kuzivunja nguvu za wafalme. Mimi nayafungua malango ya mji mbele yako, na hakuna lango litakalofungwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwa mpakwa mafuta wake, Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume kutiisha mataifa mbele yake na kuwavua wafalme silaha zao, kufungua milango mbele yake ili malango yasije yakafungwa:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Koreshi: “Wewe ni mfalme wangu niliyekuteua; mimi naitegemeza nguvu yako ili uyashinde mataifa mbele yako, na kuzivunja nguvu za wafalme. Mimi nayafungua malango ya mji mbele yako, na hakuna lango litakalofungwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hili ndilo asemalo BWANA kwa mpakwa mafuta wake, Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume kutiisha mataifa mbele yake na kuwavua wafalme silaha zao, kufungua milango mbele yake ili kwamba malango yasije yakafungwa:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hili ndilo asemalo bwana kwa mpakwa mafuta wake, Koreshi, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume kutiisha mataifa mbele yake na kuwavua wafalme silaha zao, kufungua milango mbele yake ili malango yasije yakafungwa:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Koreshi: “Wewe ni mfalme wangu niliyekuteua; mimi naitegemeza nguvu yako ili uyashinde mataifa mbele yako, na kuzivunja nguvu za wafalme. Mimi nayafungua malango ya mji mbele yako, na hakuna lango litakalofungwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyomwambia Kiro, aliyempaka mafuta: Nimemshika mkono wake wa kuume, nikanyage mbele yake mataifa mazima, nikafungua mishipi viunoni kwa wafalme, nikafungua mbele yake milango na malango, yasifungike tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi kwa Kiro, muchaguliwa wake: Nilikuchagua kuwa mufalme kwa kunitumikia. Ninaimarisha nguvu yako kusudi uyashinde mataifa mbele yako, na kuzivunja nguvu za wafalme. Mimi ninafungua milango ya muji mbele yako, na hakuna mulango utakaofungwa.