Isaiah 45:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni mimi niliyemwamuru Koreshi kuchukua hatua, atekeleze matakwa yangu. Nitazifanikisha njia zake zote; ataujenga upya mji wangu Yerusalemu, na kuwapa uhuru watu wangu walio uhamishoni, bila kutaka malipo wala zawadi.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu: nitazinyoosha njia zake zote. Yeye atajenga mji wangu upya, na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni, lakini si kwa kulipiwa fedha wala kupewa zawadi, asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni mimi niliyemwamuru Koreshi kuchukua hatua, atekeleze matakwa yangu. Nitazifanikisha njia zake zote; ataujenga upya mji wangu Yerusalemu, na kuwapa uhuru watu wangu walio uhamishoni, bila kutaka malipo wala zawadi.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu: Nitazinyosha njia zake zote. Yeye atajenga kwa upya mji wangu na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni, lakini si kwa kima cha fedha wala kwa kupewa zawadi, asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu: nitazinyoosha njia zake zote. Yeye atajenga mji wangu upya, na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni, lakini si kwa kulipiwa fedha wala kupewa zawadi, asema bwana Mwenye Nguvu Zote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni mimi niliyemwamuru Koreshi kuchukua hatua, atekeleze matakwa yangu. Nitazifanikisha njia zake zote; ataujenga upya mji wangu Yerusalemu, na kuwapa uhuru watu wangu walio uhamishoni, bila kutaka malipo wala zawadi.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nimemwamsha naye yeye (Kiro) kwa hivyo, nilivyo mwongofu, nazo njia zake zote na nizinyoshe. Yeye ndiye atakayeujenga mji wangu, nao watu wangu waliotekwa atawafungua, wajiendee; lakini havitakuwa kwa makombozi wala kwa fedha za kupenyezewa. Ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni mimi niliyemwamuru Kiro akuje, atimize mapenzi yangu. Nitazifanikisha njia zake zote. Ataujenga upya muji wangu Yerusalema, na kuwapa uhuru watu wangu wanaokuwa katika uhamisho, bila kutaka malipo wala zawadi. –Ni Yawe wa majeshi anayesema hivyo.