Isaiah 45:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu, Mungu pekee, ndiye aliyeiumba dunia, ndiye aliyeiumba na kuitegemeza. Hakuiumba iwe ghasia na tupu, ila aliiumba ikaliwe na viumbe vyake. Yeye asema sasa: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, yeye aliyeumba mbingu, ndiye Mungu; yeye aliyeifanya dunia na kuiumba, yeye ndiye aliiwekea misingi imara, hakuiumba ili iwe tupu, bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake. Anasema: “Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, wala hakuna mwingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu, Mungu pekee, ndiye aliyeiumba dunia, ndiye aliyeiumba na kuitegemeza. Hakuiumba iwe ghasia na tupu, ila aliiumba ikaliwe na viumbe vyake. Yeye asema sasa: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa hili ndilo asemalo BWANA, yeye aliyeumba mbingu, ndiye Mungu; yeye aliyeifanya dunia na kuiumba, yeye ndiye aliyeiwekea misingi imara, hakuiumba ili iwe tupu, bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake, anasema: “Mimi ndimi BWANA, wala hakuna mwingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa hili ndilo asemalo bwana, yeye aliyeumba mbingu, ndiye Mungu; yeye aliyeifanya dunia na kuiumba, yeye ndiye aliiwekea misingi imara, hakuiumba ili iwe tupu, bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake. Anasema: “Mimi ndimi bwana, wala hakuna mwingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba iwe ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu, Mungu pekee, ndiye aliyeiumba dunia, ndiye aliyeiumba na kuitegemeza. Hakuiumba iwe ghasia na tupu, ila aliiumba ikaliwe na viumbe vyake. Yeye asema sasa: “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hivi ndivyo, anavyosema Bwana aliyeziumba mbingu, yeye Mungu, aliyeifanya nchi na kuitengeneza vema, yeye aliyeishikiza, kwa kuwa hakuiumba, iwe tupu, yeye aliyeitengeneza, watu waikae, yeye anasema: Mimi ndimi Bwana, hakuna mwingine tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi ndivyo anavyosema Yawe aliyeumba mbingu, ndiye Mungu aliyeipa dunia umbo na kuifanya na kuiimarisha. Hakuiumba kusudi ibaki ukiwa, lakini aliipa umbo kusudi iikaliwe na viumbe vyake: Mimi ni Yawe, wala hakuna mwingine.