Isaiah 45:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Semeni wazi na kutoa hoja zenu; shaurianeni pamoja! Ni nani aliyetangaza zamani matukio ya sasa? Ni nani aliyetamka mambo haya zamani? Je, haikuwa mimi Mwenyezi-Mungu? Hakuna Mungu mwingine ila mimi! Mimi ni Mungu wa haki na mwokozi; hakuna mwingine ila mimi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo; wao na wafanye shauri pamoja. Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, aliyelitangaza tangu zamani za kale? Je, haikuwa Mimi, Mwenyezi Mungu? Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, Bwana? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Semeni wazi na kutoa hoja zenu; shaurianeni pamoja! Ni nani aliyetangaza zamani matukio ya sasa? Ni nani aliyetamka mambo haya zamani? Je, haikuwa mimi Mwenyezi-Mungu? Hakuna Mungu mwingine ila mimi! Mimi ni Mungu wa haki na mwokozi; hakuna mwingine ila mimi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tangazeni lile litakalokuwapo, lisemeni hilo, wao na wafanye shauri pamoja. Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, aliyetangaza tangu zamani za kale? Je, haikuwa Mimi, BWANA? Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo, wao na wafanye shauri pamoja. Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani, aliyetangaza tangu zamani za kale? Je, haikuwa Mimi, bwana? Wala hapana Mungu mwingine zaidi yangu mimi, Mungu mwenye haki na Mwokozi; hapana mwingine ila mimi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Semeni wazi na kutoa hoja zenu; shaurianeni pamoja! Ni nani aliyetangaza zamani matukio ya sasa? Ni nani aliyetamka mambo haya zamani? Je, haikuwa mimi Mwenyezi-Mungu? Hakuna Mungu mwingine ila mimi! Mimi ni Mungu wa haki na mwokozi; hakuna mwingine ila mimi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Semeni, leteni mashahidi! Na wapige shauri pamoja! Yuko nani aliyeambia watu haya, wakiyasikia huko kale? Yuko nani aliyeyatangaza tangu mwanzo? Si mimi Bwana? Hakuna tena aliye Mungu, isipokuwa mimi. Mungu aliye mwongofu na mwokozi hayuko pasipo mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutangaze na kusema habari zenu. Mufanye shauri pamoja! Ni nani aliyetangaza zamani matukio ya sasa? Ni nani aliyesema mambo haya zamani? Haikukuwa mimi Yawe? Hakuna Mungu mwingine isipokuwa mimi! Mimi ni Mungu wa haki na mwokozi; hakuna mwingine isipokuwa mimi.