Isaiah 45:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitakupa hazina zilizofichwa gizani, na mali iliyo mahali pa siri, upate kutambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ninayekuita kwa jina lako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitakupa hazina za gizani, mali iliyofichwa mahali pa siri, ili upate kujua kwamba Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitakupa hazina zilizofichwa gizani, na mali iliyo mahali pa siri, upate kutambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ninayekuita kwa jina lako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitakupa hazina za gizani, mali zilizofichwa mahali pa siri, ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimi BWANA, Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitakupa hazina za gizani, mali zilizofichwa mahali pa siri, ili upate kujua ya kwamba Mimi ndimi bwana, Mungu wa Israeli, akuitaye kwa jina lako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitakupa hazina zilizofichwa gizani, na mali iliyo mahali pa siri, upate kutambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ninayekuita kwa jina lako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitakupa malimbiko yaliyomo gizani nazo tunu zilizofichwa, kusudi upate kujua, ya kuwa mimi ni Bwana, Mungu wa Isiraeli ndiye aliyekuita kwa jina lako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakupa akiba zilizofichwa na mali inayokuwa pahali pa siri, upate kutambua kwamba mimi ni Yawe, Mungu wa Israeli, ninayekuita kwa jina lako.